Wednesday, 11 January 2017


TUMBLI APATIKANA AKIFANYA MAPENZI NA PAA


Tumbili mmoja kutoka Japan amerekodiwa katika kanda ya video akijaribu kufanya mapenzi na paa.

Watafiti walimuona mnyama huyo akijaribu kufanya mapenzi na paa wawili mnamo mwezi Novemba 2015 wakati wa msimu wa uzalishaji wa tumbili.

Tumbili hao wamekuwa wakionekana wakijaribu kuwapandia paa hao katika mchezo.

Tabia hiyo imeorodhshwa katika utafiti uliochapishwa katika jarida kuhusu nyani.

Tumbili huyo wa kiume asiye na hamu ya kufanya mapenzi na tumbili wenzake na amekuwa akiwafukuza tumbili wengine waume ambao wamekuwa wakimkaribia.

Mwanzilishi mwenza wa utafiti huo Alexandre Bonnefoy alisema: Tumbili huyo alimpanda paa huyo na kuonyesha tabia za kujamiana zilizoshirikisha tabia 15 tofauti za kufanya tendo la ngono katika kipindi cha sekunde 10 kabla ya kufanya mapenzi.

Sio mfano wa kwanza kwa wanyama tofauti kutekeleza tendo hilo.

Mwaka 2014, ripoti ya Seal kujamiana na Penguin iligonga vichwa vya habari.

No comments:

Post a Comment